IQNA

Vipindi maalumu vya mwezi wa Ramadhani katika Radio Morocco

10:34 - August 14, 2010
Habari ID: 1972422
Radio ya Kitaifa ya Morocco inatangaza vipindi maalumu vya kiutamaduni na kidini kwa mnasaba wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Kati ya vipindi mbalimbali vinavyotangazwa na radio ya taifa ya nchi hiyo ya Waislamu ya Kaskazini mwa Afrika ni qasida na mawaidha yanayowajumuisha wataalamu wa masuala ya Kiislamu na maulamaa wa ngazi za juu nchini humo. Aidha kuna mpango wa kuwepo tamthilia za radio zitakazokuwa na maudhui ya Qur'an Tukufu.
Wakuu wa Radio ya Taifa ya Morocco pia wamesema katika mwezi wa Ramadhani kutakuwepo na kiraa cha Qur'ani Tukufu kutoka kwa makari mashuhuri wa ulimwengu wa Kiislamu. Aidha waliohifadhi Qur'ani nchini humo wataalikwa studioni ili kufanya mazungumzo na wasikilizaji kote nchini humo.
632107
captcha