IQNA

Dakar, mwenyeji wa kongamano la ‘Maisha ya Ndoa katika Uislamu’

11:37 - August 14, 2010
Habari ID: 1972749
Kongamano la ‘Maisha ya Ndoa katika Uislamu’ ambalo ni katika mfululizo wa vikao vya kila mwaka vya Harakati ya Udugu na Usawa wa Kiislamu ya Senegal (MFSI) linatazamiwa kufanyika leo katika mji mkuu wa nchi hiyo Dakar.
Wanachama wa harakati ya MFSI watajadili na kubadilishana mawazo kuhusu suala la ndoa na umuhimu wa familia katika Uislamu.
Harakati ya Udugu na Usawa wa Kiislamu ya Senegal imetoa taarifa ikiwataka wananchi kushiriki katika kikao hicho cha kila mwaka na kutoa maoni yao kuhusu maudhui inayojadiliwa katika kongamano hilo.
Wahadhiri kadhaa wa vyuo vikuu watahutubia kikao hicho na hadhirina watakuwa na fursa ya kuuliza maswali ya kidini. 632230


captcha