IQNA

Kikao cha 'Ramadhani, Mwezi wa Qur'ani' chaanza Imarati

12:52 - August 15, 2010
Habari ID: 1973646
Kikao cha 'Ramadhani, Mwezi wa Qur'ani' kimeanza Jumapili ys leo tarehe 15 Agosti huko Abu Dhabi mji mkuu wa Umoja wa Falme za Kiarabu.
Kwa mujibu wa shirika rasmi la habari la umoja huo WAM kikao hicho kimeandaliwa na Kamati Kuu ya Tamasha ya Tano la Ramadhani ya mji wa Abu Dhabi kwa ushirikiano wa wanawake kadhaa wa Imarati.
Batinatu ar-Rifai mmoja wa wanawake watafiti wa Qur'ani wa Misri atazungumza katika kikao hicho kuhusu fadhila za mwezi wa Ramadhani, kuteremshwa Qur'ani katika mwezi wa Ramadhani, kunufaika na mwezi huu katika utekelezaji wa mambo mema na kujikurubisha kwa Mola Muumba.
Tunaashiria hapa kwamba tamasha hiyo ya mwezi mtukufu wa Ramadhani imekuwa ikiendelea katika mji wa Abu Dhabi tokea mwanzoni mwa mwezi huu na ratiba zake mbalimbali za Qur'ani, kidini, kiutamaduni na kijamii zitaendelea kwa muda wa wiki tatu.
Hotuba za kidini na Qur'ani, mashindano ya wasomaji bora wa kike kwa mbinu ya tarteel, kasida za kidini na vikao vya fasihi ni miongoni mwa ratiba zitakazotekelezwa katika tamasha hiyo. 632894
captcha