Benki ya kwanza ya Kiislamu nchini Ubelgiji itaanzishwa hivi karibuni huko Brussels kwa ushirikiano wa Muhammad Boliv, Mkuu wa Jumuiya ya Muslim Executive na wanauchumi kadhaa wa Kiislamu wa nchi hiyo.
Akizungumzia suala hilo hivi karibuni katika mkutano na waandishi habari, Muhammad Boliv alisema kuwa anataraji kuwa benki za nchi hiyo zitashirikiana naye katika kuanzisha benki hiyo ya Kiislamu lakini kwamba kufikia sasa wakuu wa benki hizo wamekuwa wakiamiliana naye kwa tahadhari kubwa.
Amesema, kama benki hizo hazitashirikiana naye kuhusiana na kuanzishwa kwa benki hiyo ya Kiislamu, atalazimika kuanzisha mazungumzo na mashirika ya fedha ya uchumi ya nchi za Ghuba ya Uajemi zikiwemo nchi za Kuwait na Qatar ili kufikia lengo hilo.
Muhammad Boliv amesema, tayari wameshafanya mazungumzo na wasimamizi wa Kamisheni ya Masuala ya Benki, Viwanda na Bima ya Ubelgiji na kwamba wanasubiri jibu lao la mwisho kuhusiana na kadhia hiyo. 632897