IQNA

Mashindano ya Qur'ani Tukufu yaanza Imarati

12:57 - August 15, 2010
Habari ID: 1973665
Mashindano ya Kitaifa ya Qur'ani Tukufu ya Umoja wa Falme za Kiarabu yameanza Jumapili ya leo katika Ukumbu wa Kidini na Kiutamaduni wa Turath al Imarat katika mji mkuu wa nchi hiyo Abu Dhabi.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mashindano hayo yanafanyika katika fremu ya Tamasha ya Mwezi wa Ramadhani ya taasisi ya Turath al Emarat.
Mashindano hayo yatakuwa katika vitengo viwili vya wanawake na wanaume na kwa mara ya kwanza yatafanyika kitaifa.
Wasimamizi wa mashindano hayo wanasema majaji watajumuisha maustadhi wa kiraa pamoja na maulamaa wa Kiislamu wa Imarati.
:633495
captcha