Mwandishi wa IQNA katika maonyesho hayo ameripoti kuwa kitabu hicho kina tafsiri na maelezo ya Imam Ali (as) kuhusu aya na sura za Qur’ani yaliyokusanywa kutoka kwenye vyanzo mbalimbali na kupangwa kwa kufuata mpangilio wa sura za Qur’ani Tukufu.
Kitabu hicho cha tafsiri ya Imam Ali bin Abi Twalib (as) kimetayarishwa na Sayyid Ali Aashur katika juzuu 10 na kuchapishwa na Kituo cha Utamaduni cha Mashariki ya Kati mjini Beirut, Lebanon.
Kitabu kingine kinachoonyeshwa kwa mara ya kwanza katika maonyesho ya Kimataifa ya Qur’ani ya Tehran ni Insiklopidia ya Ahlul Bait ambayo imechapishwa kwa lugha ya Kiarabu.
Kitabu hicho kimeandikwa na Mahdi Khalil Ja’far na kinakusanya maarifa kamili kuhusu Ahlu Baiti kuanzia Mtume Muhammad (saw) hadi Imam wa Zama (as). Kitabu hicho kina juzuu 16. 634126