IQNA

Tafsiri ya Qur’ani ya Imam Ali (as) katika Maonyesho ya Kimataifa ya Qur’ani Tehran

15:40 - August 16, 2010
Habari ID: 1974799
Tafsiri ya Qur’ani iliyokusanywa kutokana na hotuba za Imam Ali bin Abi Twalib (as) inaonyeshwa katika chumba cha Athari za Utafiti wa Qur’ani katika Ulimwengu wa Kiislamu kwenye maonyesho ya Kimataifa ya Qur’ani ya Tehran.
Mwandishi wa IQNA katika maonyesho hayo ameripoti kuwa kitabu hicho kina tafsiri na maelezo ya Imam Ali (as) kuhusu aya na sura za Qur’ani yaliyokusanywa kutoka kwenye vyanzo mbalimbali na kupangwa kwa kufuata mpangilio wa sura za Qur’ani Tukufu.
Kitabu hicho cha tafsiri ya Imam Ali bin Abi Twalib (as) kimetayarishwa na Sayyid Ali Aashur katika juzuu 10 na kuchapishwa na Kituo cha Utamaduni cha Mashariki ya Kati mjini Beirut, Lebanon.
Kitabu kingine kinachoonyeshwa kwa mara ya kwanza katika maonyesho ya Kimataifa ya Qur’ani ya Tehran ni Insiklopidia ya Ahlul Bait ambayo imechapishwa kwa lugha ya Kiarabu.
Kitabu hicho kimeandikwa na Mahdi Khalil Ja’far na kinakusanya maarifa kamili kuhusu Ahlu Baiti kuanzia Mtume Muhammad (saw) hadi Imam wa Zama (as). Kitabu hicho kina juzuu 16. 634126

captcha