IQNA

Mashindano ya 18 ya Qur’ani kufanyika nchini Senegal

17:50 - August 17, 2010
Habari ID: 1975770
Mashindano ya kieneo ya 18 ya kuhifadhi Qur’ani ya Senegal yatafanyika Jumapili ijayo katika mji wa Tiyas.
Shirika rasmi la habari la Senegal (APS) limeripoti kuwa mashindano hayo yatasimamiwa na Jumuiya ya Vijana wa Kiislamu ya Senegal (UJMS) kwa ushirikiano wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kutangaza Uislamu katika uwanja wa michezo wa Lat Dior mjini Tiyas.
Mashindano hayo yatavishirikisha vituo zaidi ya 40 vya Qur’ani na washiriki watashindana katika nyanja za kuhifadhi Qur’ani kamili, juzuu 15, kuhifadhi hizbu 30 za Qur’ani na maarifa jumla ya kitabu hicho cha Mwenyezi Mungu.
Sherehe za ufunguzi wa mashindano hayo zitahudhuriwa na Rais Abduolaye Wade wa Senegal, Meya ya mji wa Tiyas, mabalozi wa nchi za Kiislamu nchini Senegal na viongozi mbalimbali wa kidini. 635333
captcha