Mwenyekiti wa kamati inayosimamia mashindano hayo Ali Ahmad al Bariq amesema kuwa mashindano ya sasa yanafanyika katika viwango vya kuhifadhi Qur’ani kamili, kuhifadhi juzuu 25, juzuu 20, juzuu 15, juzuu 10 na juzuu 5.
Ameongeza kwamba zawadi ya riyali elfu 40 za Qatar itatolewa kwa washindi wa kwanza.
Ali Yusuf ambaye ni miongoni mwa majaji wa mashindano hayo amesema: “Mashindano haya yanafanyika kwa shabaha ya kuwahamasisha wanajeshi kuhifadhi Qur’ani Tukufu.” Amesisitiza kuwa ili kuwahamasisha zaidi wanajeshi kushiriki kwenye mashindano ya Qur’ani, washindi wa kwanza mbali ya kupewa zawadi ya kitita cha fedha watadhaminiwa safari ya kwenda kutekeleza ibada ya hija na umra. 636123