Sherehe za ufunguzi wa mashindano hayo zimehudhuriwa na mtawala wa Dubai Muhammad bin Rashind Al Maktum, shakhsia wa kidini, mabalozi wa nchi za Kiislamu na viongozi wa kieneo.
Washiriki kutoka ulimwengu wa Kiislamu na nchi zenye idadi ndogo ya Waislamu wanashiriki katika mashindano hayo yanayofanyika katika sekta ya kuhifadhi Qur’ani.
Kamati inayosimamia mashindano ya Qur’ani ya Dubai imetayarisha zawadi nono kwa washindi wa mashindano hayo.
Kabla ya kuanza mashindano hayo kulitekelezwa ratiba za kiutamaduni na kulitolewa hotuba za kidini katika Chumba cha Biashara na Viwanda cha Dubai. 636093