Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Idara ya Miongozo ya Kidini na Mafundisho ya Qurani katika Wizara ya Waqfu na Masuala ya Kiislamu ya Algeria imetoa taarifa na kusema: “Mashindano haya yatafanyika chini ya usimamizi wa Rais wa Algeria Abdulaziz Bouteflika na yatashirikisha nchi 41 wanachama wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu . Washiriki watakuwa chini ya umri wa miaka 25”.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa : “Jopo la majaji litajumuisha Maustadhi watatu kutoka Algeria, Libya na Iran”.
Zawadi za mashindano hayo ya kimataifa ya Quran nchini Algeria yatakuwa kama ifuatavyo: Nafasi ya kwanza Milioni Dinari milioni moja, nafasi ya pili Dinari laki nane na nafasi ya tatu dinari laki sita.
636244