Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, jimbo la Queensland la Australia ambalo lina msimu wa baridi wenye jua linakusudia kuwavutia watalii kutoka Mashariki ya Kati. Kutokana na hali hiyo ya kijiografia wakuu wa jimbo hilo wameamua kujenga eneo maalumu kwa Waisalmu wanaofunga ili kuwavutia katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Mkuu wa idara ya utalii ya Queensland Paul Buggy amesema hoteli nyingi katika eneo hilo sasa zinajenga vyumba maalumu vya sala kwa ajili ya Waislamu na kwamba kituo maalumu cha mwezi wa Ramadhani kimejengwa katika eneo hilo ili kuwavutia Waislamu wengi zaidi.
636677