IQNA

Dharau ya afisa wa Sweden dhidi ya Waislamu

15:08 - August 21, 2010
Habari ID: 1977885
Henrick Emilson, Mshauri wa Masuala ya Wahajiri katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Sweden ameshambulia Uislamu na Waislamu katika tovuti yake.
Afisa huyo ameandika makala katika tovuti yake akiufananisha Uislamu na ukomunisti huku akiwatuhumu Waislamu kuwa ni watu wa kutumia mabavu. Afisa huyo wa serikali ya Sweden vilevile ameutusi Uislamu kwa kuiita dini hii tukufu ya Mwenyezi Mungu kuwa ni dini ya shari na kuwaita Waislamu kuwa ni washari.
Hatimaye afisa huyo wa Sweden amelazimika kufuta makala hiyo kwenye tovuti hiyo baada ya kukabiliwa na ukosoaji na lawama kali za jamii ya Waislamu wa nchi hiyo kufuatia tuhuma hizo kuchapishwa na kusambazwa kwa wingi na magazeti muhimu ya nchi hiyo. 637342
captcha