Mashindano hayo yameandaliwa na Kamati ya Hilal ya Masuala ya Kijamii na Kiutamaduni ya mjini Riadh, mji mkuu wa Saudia. Kwa mujibu wa tofuti ya kamati hiyo ya alhilalclub.com, mashindano hayo yanafanyika katika sehemu tatu za kuhifadhi na kusoma Qur'ani nzima, kuhifadhi na kusoma juzuu 5 tokea sura ya al-Ahqaaf hadi mwisho wa sura ya an-Nas na mwishowe kuhifadhi juzuu ya 29 na 30 maalumu kwa washindani walio na umri wa chini ya miaka 13.
Kamati ya Hilal imewataka walio na hamu ya kushiriki katika mashindano hayo kuyatembelea makao makuu yao mjini Riadh.
Mashindano hayo yanafanyika katika fremu ya ratiba na shughuli maalumu za kidini na kiutamaduni za kamati hiyo katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani. 637351