IQNA

Kituo kipya cha Kiislamu, Madrassa na Msikiti Zanzibar

15:19 - August 21, 2010
Habari ID: 1977955
Shirika moja la Uturuki limefadhili ujenzi wa kituo kipya cha Kiislamu, Msikiti na Madrassa katika Visiwa vya Zanzibar nchini Tanzania.
Kwa mujibu wa tovuti ya Haber 7, taasisi hizo tatu za Kiislamu zimejengwa kwa kwa himaya ya Jumuiya ya Uturuki ya Haki na Uhuru wa Binaadamu (İHH).
Sherehe za Ufunguzi taasisi hizo za Kiislamu zimehudhuriwa na Naibu Waziri Kiongozi wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar Ali Juma Shamhuna.
Akizungmza katika sherehe hizo kijijini Muangani Zanzibar, Shamhuna amesema: “Madrassa hii ni kumbukumbu ya Faruk Aktaş mmoja kati ya wanachama wa Jumuiya ya Uturuki ya Haki na Uhuru wa Binaadamu ambaye alipoteza maisha yake katika juhudi za kutuma misaada Afghansitan”. Amesema Madrassa hiyo itatoa mafunzo kwa lugha za Kiarabu na Kiingereza.
Ali Juma Shamhuna ametoa shukrani zake kwa serikali ya Uturuki na shirika la İHH kwa kuwasaidia watu wa Zanzibar. Ameelezeka matumaini yake kuwa kituo hicho kipya cha Kiislamu kitatoa machango mkubwa katika kuinua utamaduni wa Kiislamu visiwani Zanzibar.
637400
captcha