Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, ufunguzi huo wa Jumamosi usiku pia ulihudhuriwa na Dkt. Mahdi Mostafavi Mkuu wa Shirika la Utamaduni na Uhusiano wa Kiislamu la Iran.
Kati ya nchi zinazoshiriki katika kitengo cha kimataifa cha maonyesho ya kimataifa ya Qur'ani ni pamoja na Pakistani, Tunisia, Kyrgyzstan, Bangladesh, Lebanon, Kuwait, Bosnia Herzegovina, Syria, India, Afghanistan, Thailand na Uturuki.
Washiriki kutoka nchi hizo wanaojumuisha wasomi na wasanii wanaonyesha athari kama vile kaligrafia ya Qur'ani Tukufu, vitabu vya taaluma ya Qur'ani n.k.
Maonyesho ya 18 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu yalianza tarehe 27 mwezi wa Shaaban na yataendelea hadi tarehe 23 ya mwezi mtukufu wa Ramadhani. 638452