IQNA

Mashindano ya kwanza ya utafiti katika Qur'ani Tukufu kufanyika New York

11:41 - August 22, 2010
Habari ID: 1978393
Mashindano ya kwanza ya kila mwaka ya utafiti katika Qur'ani Tukufu, maalumu kwa familia za Kiislamu zinazoishi nchini Marekani yatafanyika hivi karibuni mjini New York.
Mashindano hayo yameandaliwa na Kituo cha Shia Ithna-Asheri kilichoko katika mji huo. Kwa mujibu wa tovuti ya kituo hicho 'Sijny' mashindano hayo yameandaliwa kwa madhumuni ya kunyanyua kiwango cha maarifa ya Qur'ani katika familia za Waislamu na kuwashajiisha wawe na hamu ya kusoma na kuzingatia kitabu hicho kitakatifu.
Kituo kilichotajwa cha Kiislamu kimekuwa kikiweka maswali ya Qur'ani katika kurasa za tovuti yake na kuwataka walio na hamu ya kuyajibu, wayajibu na kisha kuchunguzwa na wasimamizi husika wa kituo hicho. Washindi wamepangiwa kutunukiwa zaidi katika siku ya Idulfitr. 638283
captcha