IQNA

Tamasha ya Ramadhani yafanyika katika mji mkuu wa Indonesia

11:31 - August 22, 2010
Habari ID: 1978394
Tamasha ya mwezi mtukufu wa Ramadhani imekuwa ikiendelea katika siku hizi za Ramadhani huko Jakarta, mji mkuu wa Indonesia.
Kwa mujibu wa tovuti ya beritajakarta, tamasha hiyo ililoanza siku ya Ijumaa tarehe 20 Agosti itaendelea hadi Jumapili tarehe 29 ya mwezi huu. Sanaa mbalimbali za Kiislamu zinaonyeshwa katika tamasha hiyo iliyoandaliwa na Taasisi Kuu ya Jakarta.
Akizungumzia suala hilo, Ghazali, mkuu wa kitengo cha utamaduni cha taasisi hiyo amesema, likiwa ni nembo ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, tamasha hiyo imekusudia kuonyesha na kusambaza sanaa ya Kiislamu katika jamii ya Indonesia. Amesema ratiba mbalimbali za sanaa, kijamii, kidini na hutoba pamoja na vikao vya mazungumzo kuhusu mwezi mtukufu wa Ramadhani, msaada kwa watoto wasio na walezi na familia masikini ni miongoni mwa mipango itakayotekelezwa katika tamasha hilo. 638546
captcha