IQNA

Maudhui za vikao vya mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya Libya zatangazwa

16:00 - August 22, 2010
Habari ID: 1978836
Jumuiya ya masuala ya kheri ya Wa'tasamu ya Libya imetangaza maudhui za mijadala ya vikao vya taaluma ya Qur'ani vitakavyofanyika pambizoni mwa Mashindano ya 6 ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur'ani Tukufu makhsusi kwa wanawake ya jumuiya hiyo.
Jumuiya ya Wa'tasimu imetangaza kuwa miongoni mwa maudhui zitakazojadiliwa ni pamoja na Muujiza wa Kielimu wa Qur'ani na Suna za Mtume (saw), Nafasi ya Mwanamke katika Uislamu, Sisi na Qur'ani, Kuteremeshwa Qur'ani na Mawasiliano Baina ya Ardhi na Mbingu, Jihadi ya Nafsi na Kupambana na Shetani, Wajibu Wetu Mkabala wa Msikiti wa al Aqsa na Palestina, Mtume wa Rehma na kadhalika.
Wanawake 58 kutoka nchi mbalimbali za Kiafrika, Asia na Ulaya watashiriki katika mashindano hayo.
Mshindani mkongwe zaidi katika mashindano hayo ana umri wa amiaka 52 kutoka Italia na mdogo kuliko wote ni Latifa Mustafa Saidi kutoka Msumbiji na Khadija Ahmad al Nour wa Chad ambao wana umri wa miaka 13.
Mashindano ya 6 ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur'ani makhusi kwa ajili ya wanawake ya Libya yataanza Ijumaa ya tarehe 27 Agosti na kumalizika Jumatatu tarehe 30. 638702


captcha