IQNA

Kongamano la "Amani na Matumaini" kufanyika nchini Marekani

15:59 - August 22, 2010
Habari ID: 1978838
Viongozi wa dini mbalimbali katika jimbo la Florida huko Marekani wanakusudia kujibu uamuzi uliochukuliwa na kanisa la The Dove World Outreach Center la mji huo wa kuchoma moto kitabu kitakatifu cha Qur'ani kwa kuitisha kongamanao la "Amani na Matumaini".
Kongamano hilo linatarajiwa kufanyika tarehe 10 Septemba likihudhuriwa na viongozi wa dini za Uislamu, Ukristo, Uyahudi na Hindu katika jimbo la Florida nchini Marekani.
Kasisi Don Johnson wa Marekani amelaani wito wa kanisa hilo wa kuchomwa moto kitabu kitukufu cha Qur'ani na akasema lengo la kuitishwa kongamano hilo ni kuimarisha maelewano, kuheshimiana, amani na kutambuliwa rasmi itikadi za watu wengine.
Katika upande mwingine mkuu wa kanisa la The Dove World Outreach Center Terry Jones katika jimbo la Florida ameendelea kusisitiza juu ya misimamo yake ya kupiga vita Uislamu na kufanya mikakati ya kuitisha sherehe ya kuchomwa moto Qur'ani siku ya tarehe 11 Septemba.
Kasisi Jones amewaandikia barua viongozi wa serikali ya jimbo la Florida akitaka waruhusu sherehe za kuchomwa moto Qur'ani lakini ombi hilo limekataliwa. 638841
captcha