IQNA

Cyprus yapinga kutia nanga meli ya misaada ya Maryam katika bandari zake

11:47 - August 23, 2010
Habari ID: 1979150
Kufuatia uamuzi wa viongozi wa Cyprus wa kuzuia meli ya Maryam iliyosheheni misaada ya kibinadamu kwa ajili ya watu wa Ukanda wa Gaza walio chini ya mzingiro wa kidhulma wa utawala ghasibu wa Israel, wanaharakati wa haki za binadamu wameamua kubadili njia ya meli hiyo na kuielekeza Ugiriki.
Meli ya Maryam ilitarajiwa kuondoka katika bandari ya Tripoli nchini Lebanon na kuelekea Cyprus hapo jana Jumapili na kisha kuelekea Gaza, laini viongozi wa serikali ya Cyprus wakapinga vikali jambo hilo.
Meli ya Maryam imewabeba wanaharakati wa haki za binadamu kutoka Lebanon na nchi nyinginezo za Ulaya na Marekani kwa ajili ya kuwafikishia misaada ya dharura ya kibinadamu wakazi wa Ukanda wa Gaza wanaoishi chini ya mzingiro wa Wazayuni wa Israel. 638989
captcha