IQNA

Awamu ya tatu ya mashindano ya Qur’ani ya Imarati kuanza leo

15:13 - August 23, 2010
Habari ID: 1979581
Awamu ya tatu ya mashindano ya kusoma Qur’ani makhsusi kwa wanaume imeanza Jumatatu ya leo katika mji mkuu wa Imarati Abu Dhabi.
Shirika rasmi la habari la Imarati limeripoti kuwa mashindano hayo ni sehemu ya Tamasha ya Ramadhani ya klabu ya masuala ya kidini na kitamaduni ya Turathul Imarat.
Mashindano hayo yana sehemu tano na sehemu hii ya tatu ina makundi mawili ya vijana wenye umri wa kati ya miaka 7 hadi 15 na kundi la pili ni la vijana wenye umri wa miaka 16 hadi 30.
Awamu hii ya mashindano ya Qur’ani inasimamiwa na kamati ya majaji kadhaa wanaoongozwa na Ibrahim al Janabi.
Awamu ya kwanza ya mashindano ya kusoma Qur’ani ya Imarati ilianza Jumatatu ya wiki iliyopita. 639483
captcha