IQNA

Tarjumi 112 za Qur'ani katika maonyesho ya Tehran

12:48 - August 24, 2010
Habari ID: 1979765
Kitengo cha tarjumi ya Qur'ani Tukufu katika Maonyesho ya 18 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Tehran kimefanikiwa kuarifisha tarjumi za Qur'ani Tukufu kwa lugha 112 za dunia.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA kila tarjumi imetengewa ubao maalumu unaotoa maelezo kuhusu tarjuma husika. Maelezo hayo yanajumuisha lugha ya tarjumi, nchi, idadi ya wazungumzaji wa lugha husika, idadi ya Waislamu katika nchi husika na idadi ya tarjumi zilizowahi kuchapishwa. Aidha kuna maelezo kuhusu mtarjumi wa kwanza na tarehe ya tarjumi ya kwanza ya Qur'ani.
Kati ya tarjuma zilizo katika maonyesho hayo ni za lugha kama vile Kiswahili, Kiingereza, Kifaransa, Kiganda, Kishona, Kikuyu, Kihausa, Kitaliano, Kiamhari n.k.
Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Tehran yalianza tarehe 27 Shaaban na yanatazamiwa kuendelea hadi tarehe 23 ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.
640052

captcha