Kwa mujibu wa gazeti la as-Sharqul Ausat, taasisi hiyo ya kimataifa iliyo na makao makuu yake mjini New York Marekani, imetoa taarifa ikisema kuwa hatua ya kasisi huyo ya kutaka kuchoma moto hadharani Qur'ani Tukufu ni kitendo hatari, kosa kubwa na dharau ya wazi kwa matukufu ya kidini.
Taarifa hiyo imesisitiza kwamba viongozi wa madhehebu zote za Kikristo pamoja na wafuasi wa dini hiyo kote ulimwenguni wanapinga na kulaani vikali kitendo hicho cha dharau. Tunakumbusha hapa kuwa hatua ya kasisi huyo imeamsha hasira kubwa ya Waislamu, taasisi za Kiislamu pamoja na wafuasi wa dini mbalimbali duniani. 641195