Duru za kisheria zimetangaza kuwa viongozi wa Saudia wamemwachia huru Yusuf Muhammad Zahri ambaye ni mwanaharakati wa Kishia katika mji wa al Awwamiyyah ambaye alikuwa korokoroni kwa karibu miezi 8.
Muhammad Zahri alitiwa nguvuni katika mkusanyiko wa watu waliokutana katika mji wa al Awwamiyyah kupinga utendaji wa serikali ya Riyadh katika matukio ya Baqi'i mjini Madina. Mwanaharakati huyo alikamatwa na kutiwa jela bila ya kufikishwa mahakamani.
Askari usalama wa Saudi Arabia pia wamemuachia huru Ahmad Ali al Juwaihir, mwanaharakati wa Kishia katika mji wa Dammam ambaye amekuwa jela kwa kipindi cha miezi 6.
Ni vyema kukumbusha hapa kuwa maelfu ya Waislamu wa madhehebu ya Shia walipingwa na kudhalilishwa na askari usalama wa Saudi Arabia mwaka jana mjini Madina walikokwenda kuzuru kaburi la Mtume (saw), Maimamu katika kizazi chake na masahaba zake katika eneo la Baqi'i. Hatua hiyo ya askari usalama wa Saudia ilipingwa vikali na Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini humo. 640279