Kwa mujibu wa IslamRF, mashindano hayo ambayo yatakuwa ya usomaji Qur'ani yameandaliwa kwa ushirikiano wa Baraza la Mamufti wa Russia, Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO. Wawakilishi wa nchi za Kiislamu na wa jumuiya za Waislamu katika nchi zisizo za Kiislamu watashiriki katika mashindano hayo.
UNESCO inashiriki katika uandaaji wa mashindano hayo kutokana na kuwa yanasaidia kuwajumuisha Waislamu katika jamii ya Russia na wakati huo kueneza mafundisho na utamaduni wa Kiislamu nchini humo.
Mashindano hayo yamekuwa yakifanyika mjini Moscow tokea mwaka 2000. Katika mwaka huo, mashindano hayo yaliwajumuisha wanafunzi na wanachuo wa Russia tu katika msikiti wa Ijumaa wa Moscow. Hatimaye yalianza kufanyika kitaifa mwaka 2005 na kisha kutangazwa na mamufti wa Russia kuwa ya kimataifa mwaka 2007. 641695