Kwa mujibu wa wasimamizi wa kituo hicho, ratiba hizo maalumu zinatazamiwa kuanza kutekelezwa leo Jumapili, Jumanne na Alkhamisi za wiki hii tokea saa moja na nusu hadi tano na dakika 45 kwa wakati wa Vienna.
Baadhi ya ratiba zitakazotekelezwa ni pamoja na kutolewa futari, usomaji wa dua ya Jaushan Kabir, usomaji wa Qur'ani, mawaidha kutoka kwa Hujjatul Islam wal Muslimeen Aali na kisha kufanyika maombolezo maalumu ya kukumbuka kuuawa shahidi Imam Ali bin Abi Twalib (as). 643370