IQNA

Siku ya Quds ni siku ya mwamko wa Waislamu duniani

15:20 - August 30, 2010
Habari ID: 1984525
Siku ya Quds ambayo huadhimishwa Ijumaa ya Mwisho ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani imetajwa kuwa siku ya mwamko na kupata utambulisho Waislamu kote duniani.
Mtaalamu wa masuala ya kisiasa Hussein Shafi’i katika mahojiano na IQNA amesema kuwa Imam Khomeini (MA) alianza harakati za kuhuisha Uislamu kwa kuleta mwamko miongoni mwa Waislamu duniani.
Itakumbukwa kuwa Siku ya Kimataifa ya Quds ilianzishwa na muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hayati Imam Khomeini MA kama njia ya kutangaza mfungamano na taifa la Palestina na vile vile kuashiria umuhimu wa Quds Tukufu kwa Waislamu. Siku ya Kimataifa ya Quds hufanyika kila mwaka katika Ijumaa ya mwisho ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na washiriki mbali na kutangaza kufungamana kwao na taifa linalodhulumiwa la Palestina vile vile hulaani jinai za Wazayuni hasa ukaliaji wake mabavu wa Quds Tukufu.
643916
captcha