IQNA

Kadhia ya Quds itatatuliwa tu kwa umoja wa Kiislamu

12:14 - August 31, 2010
Habari ID: 1984845
Kadhia ya Quds na vile vile kadhia nyinginezo za Ghaza, Iraq, Lebanon, Afghanistan na maeneo mengine yanayodhulimiwa ya ulimwengu wa Kiislamu zitatatuliwa tu kupitia umoja wa Waislamu, mapambano na mwamko.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya mkutano wa Jumuiya ya Umoja wa Wanachuo wa Ulimwengu wa Kiislamu uliomalizika Jumapili mjini Tehran.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa iwapo ulimwengu wa Kiislamu ungekuwa na umoja na busara Waingereza hawangeweza kuupandikiza utawala haramu wa Israel katika ardhi za Palestina. Washiriki wa kongamano hilo wamesisitiza kuwa iwapo Waislamu wote duniani watarejea kikamilifu katika mafundisho ya Qur'ani Tukufu, utawala wa Kizayuni wa Israel utaangamia. Jumuiya ya Umoja wa Wanachuo wa Ulimwengu wa Kiislamu pia imetoa wito kwa Waislamu duniani kujiepusha na mifarakano na badala yake kuungana katika kukabiliana na maadui wa Uislamu. 645130
captcha