IQNA

Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Misri yaanza

12:08 - August 31, 2010
Habari ID: 1984846
Mashindano ya 12 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Misri yameanza katika mji mkuu wa nchi hiyo Cairo na yanahudhuriwa na washiriki 104 kutoka nchi 68 dunani.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mashidano hayo yalianza rasmi Jumamosi tarehe 28 Agosti katika sherehe zilizohudhuriwa na Waziri Mkuu wa Misri Ahmad Nadhif, Sheikh wa Al Azhar Ahmad al Tayyib, Mufti wa Misri Sheikh Ali Gomaa, Waziri wa Waqfu na Masuala ya Kiislamu Mahmoud Hamdi Zakzuk pamoja na mabalozi wa nchi za Kiarabu na Kiislamu.
Akizungumza katika hafla hiyo Mahmoud Hamdi Zakzuk amesema mashindanyo hayo yatajumuisha kuhifadhi Qur'ani nzima, tajwid, tartil na tafsiri ya Juzuu ya 16 ya Qur'ani. Ameongeza kuwa vile vile kutakuwa na mashindano ya kuhifadhi Juzuu 20, Juzuu 10 na Juzuu 6 za Qur'ani Tukufu.
Akizungumza katika hafla hiyo, Sheikh wa Al Azhar Ahmad al Tayyib ametoa wito kwa Waislamu kuzingatia Qur'ani Tukufu na kutekeleza mafunzo yake katika maisha yao ya kila siku.
645039
captcha