Kwa mujibu wa gazeti la nchi hiyo la al-Ittihad, mashindano hayo yanafanyika katika fremu ya ratiba maalumu za mwezi mtukufu wa Ramadhani za duru ya tano ya tamasha ya Ramadhani iliyoratibiwa na Klabu ya Masuala ya Kidini na Kiutamaduni ya Turathi za Imarati.
Mashindano hayo ambayo ni ya wanaume tu yanawashirikisha vijana wadogo walio na umri wa kati ya miaka 7 hdi 15 na vijana walio na umri wa miaka 16 hadi 30. Kamati kuu inayosimamia tamasha hiyo imepanga sherehe maalumu ya kuwazawadia washindi wa mashindano hayo ambayo itafanyika leo alasiri.
Washindi wa kwanza hadi tano wa kundi la vijana watepewa zawadi ya dirhamu za Imarati 20,000, 15,000, 10,000, 8000, na 5000 kwa utaratibu. Washindi vijana walio na umri mdogo watapewa diramu 15,000, 10,000, 8000, 5000 na 5000. 644674