IQNA

Maonyesho ya mabango yenye maudhui ya holocaust katika maonyesho ya Qur'ani

17:08 - September 02, 2010
Habari ID: 1986021
Maonyesho ya mabango yaliyo na maudhui ya holocaust au kwa ibara nyingine, mauaji ya umati yanayodaiwa kutekelezwa dhidi ya Mayahudi, Beitul Muqaddas na Masjidul Aqswa yatazinduliwa hivi karibuni katika maonyesho ya kimataifa ya Qur'ani yanayoendelea mjini Tehran, kwa ajili ya kuwaelimisha watu kuhusiana na hatari ya Uzayuni.
Mabango hayo yana maandishi yanayobainisha hatari ya vyombo vya habari pamoja na mashirika ya kimataifa ya Wazayuni. Maonyesho hayo pia yana mabango makubwa yanayoashiria hatari ya mgawanyiko unaosababishwa miongoni mwa Waislamu na Mawahabi. Sehemu inayohusiana na njama za Mawahabi inachunguza kwa kina harakati ya Mawahabi tokea itikadi hadi jinai zao katika kipindi chote cha historia, nafasi ya Wazayuni katika kuanzisha kundi hilo, harakati za Mawahabi katika kubuni na kutekeleza siasa za nje nchini Saudia na uhusiano wao na nchi za Kiislamu, msaada wao kwa makundi ya kigaidi, likiwemo la Jundullah nchini Iran na Taliban na al-Qaida katika nchi za Pakistan na Afghanistan na vilevile uungaji mkono wao kwa makundi hayo kupitia vyombo vya habari.
Siasa za chuki za kundi hilo dhidi ya Ushia pia zimechunguzwa pia katika maonyesho hayo. 646555
captcha