IQNA

Kutengenezwa nchezo ulio dhidi ya Uislamu nchini Austria

11:54 - September 04, 2010
Habari ID: 1986642
Chama chenye misimamo ya kupindukia cha Wapigania Uhuru nchini Austria FPO kimetengeneza mchezo wa kumpyuta ulio dhidi ya Uislamu unaoitwa Moschee Baba ikiwa ni katika harakati za kampeni zake za uchaguzi wa serikali za mitaa nchini humo.
Kwa mujibu wa gazeti la Zaman la nchini Uturuki, chama hicho ambacho kinapinga vikali kujengwa misikiti nchini Austria kinaonyesha katika mchezo wake huo ambao tayari unauzwa masokoni muadhini wa msikiti akishambuliwa. Mwishoni mwa mchezo huo, ibara inayosema, 'misikiti na minara imejaa Austria, kwa hivyo kama wewe inapinga Uislamu kipigie kura chama cha Wapigania Uhuru.'
Katika sehemu nyingine ya mchezo huo fursa ya utoaji maoni kuhusiana na marufuku ya ujenzi wa misikiti na minara na vilevile hijabu imetolewa kwa wachezaji wa mchezo huo.
Katika hali ambayo watengenezaji wa mchezo huo wanadai kuwa lengo lao ni kuwafanya vijana wa nchi hiyo wazingatie zaidi masuala ya siasa za nchi, chama kingine cha nchi hiyo cha Kijani tayari kimekishtaki chama hicho kwa kudharau matukufu ya kidini.
Wawakilishi wa jumuiya za Kiislamu za Austaria wamewataka viongozi husika wa serikali kuusimamisha mara moja mchezo huo pamoja na hatua za chuki dhidi ya Uislamu za chama cha Wapigania Uhuru kwa kuwa zinachochea ghasia miongoni mwa wafuasi wa dini tofauti nchini. 647019
captcha