IQNA

Siku ya mwisho ya maonyesho ya Qur'ani ya Tehran

14:17 - September 04, 2010
Habari ID: 1986933
Siku ya mwisho ya Maonyesho ya 18 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu mjini Tehran imetambuliwa kuwa siku iliyokuwa na idadi kubwa zaidi ya watu waliotembelea maonyesho hayo.
Wimbi kubwa la watu lilimiminika jana katika maonyesho hayo hususan katika kipindi cha kabla ya futari na swala ya Magharibi.
Baadhi ya sehemu za maonyesho hayo zilijaa kiasi kwamba ilikuwa vigumu kwa watu kutembelea vyumba vya maonyesho hayo.
Maonyesho ya 18 ya Kimataifa ya Qur'ani yalianza tarehe 8 Agosti na yalimalizika jana jioni.
Maonyesho hayo yalijumuisha sehemu za uchapishaji wa vitabu, taasisi za elimu na vyuo vikuu, kitengo cha teknolojia ya mawasiliano, elimu na utafiti, kitengo cha mazungumzo na mijadala ya Qur'ani, watoto, na vijana, familia, fasihi na mashairi, tarjumi ya Qur'ani, sanaa za michoro, picha na kadhalika. 647205


captcha