IQNA

Mafunzo ya "Tilawa ya Qur'ani kwa njia ya elektroniki" katika intaneti

14:22 - September 04, 2010
Habari ID: 1987021
Jumuiya ya Kuhifadhi Qur'ani ya mkoa wa Al Jubail wa Saudi Arabia imeanzisha mafunzo ya tilawa ya Qur'ani Tukufu kwa njia ya intaneti kwa wapendao kushiriki kutoka eneo lolote duniani.
Kwa mujibu wa Khalid Al Jabri Mkuu wa Jumuiya ya Kuhifadhi Qur'ani ya Al Jubail, watu wengi wapendao kujifunza tilawa ya Qur'ani Tukufu hawawezi kufanya hivyo kutokana na ukosefu wa waalimu na kwa kuzingatia hilo ndio maana umechukuliwa uamuzi wa kuanza kutoa mafunzo ya kusoma Qur'ani kwa njia ya elektroniki. Amesema mfumo huu mpya wa kutoa mafunzo utawezesha idadi kubwa zaidi ya watu kujifunza kusoma Qur'ani Tukufu.
Ameongeza kuwa hivi sasa kuna wanafunzi 8510 wanaojifunza Qur'ani katika jumuiya hiyo.
647097
captcha