IQNA

Mashindano ya Qur'ani yafanyika Tanzania

11:47 - September 05, 2010
Habari ID: 1987396
Mashindano ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu yamefanyika nchini Tanzania kwa himaya ya idara ya Jumuiya ya Kimataifa ya Ulinganio wa Kiislamu nchini humo.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA mjini Dar-es-Salaam aliyenukulu tovuti ya arabic.islamic-call , mashindano hayo yamefanyika kwa ushirikiano wa Radio Sauti ya Qur'an ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata). Mashindano hayo yamewashirikisha vijana 158 wa kike na kiume walio na umri wa kuanzia miaka minane hadi 16.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, kulikuwa na washiriki 10 waliohifadhi Qur'ani nzima, 20 katika kiwango cha kuhifadhi Juzuu 10 huku 36 wakishiriki katika kiwango cha kuhifadhi Juzuu tano na wengine 93 wakishiriki katika kiwango cha kuhifadhi Juzuu 3.
Sherehe za kuwazawadia walioshinda zilihudhuriwa Waislamu wengi wa Tanzania katika mji mkuu Dar-es-Salaam.
647118
captcha