IQNA

Mashindano ya kuhifadhi Qur'ani yaanza Kuwait

12:51 - September 05, 2010
Habari ID: 1987763
Mashindano ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu yalianza jana Jumamosi huko katika eneo la ar-Riqa nchini Kuwait huku yakiwashirikisha washindani 76 walio na umri tofauti.
Kwa mujibu wa gazeti la nchi hiyo la ar-Rai, mashindano hayo yameandaliwa na jumuiya ya kidini na kiutamaduni ya ar-Riga ya nchini Kuwait na kwa ushirikiano wa Taasisi ya Kuhuisha Turathi za Kiislamu.
Barikan al-Ajmi, mwanachama wa Baraza la Idara ya ar-Riqa ambaye pia ni msimamizi wa mashindano hayo amesema kuhusu jambo hilo kwamba mashindano hayo yamegawanywa katika makundi matatu ambapo kundi la kwanza litasoma hifdhi ya sura za Naba na Abasa, kundi la pili sura za Tahreem na Mulk na la tatu sura za Kahf na Luqman.
Amesema lengo la mashindano hayo ni kuwashajiisha vijana wa umri tofauti waweze kuhifadhi, kutadabari na kutekeleza misingi na mafundisho ya Qur'ani Tukufu. 647754
captcha