Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, tamasha hilo limefanyika katika mji wa Al Saf kwa himaya ya jumuiya ya Qur'ani ya mji huo. Tamasha hilo la Jumapili lilihudhuriwa na wanazuoni wa Chuo Kikuu cha al Azhar na wawakilishi wa Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Misri na vilevile maulama wa Qur'ani wa Misri.
Mkuu wa Jumuiya ya Qur'ani ya mji wa Al Sad Sami Ismail Elam amesema: "Mahafidhi wa Qur'ani wametunukiwa nishani na zawadi za kifedha na 100 kati yao wametunukiwa zawadi maalumu".
649815