IQNA

Kikao cha 'Uislamu, Ulaya na Utandawazi' nchini Ufaransa

12:16 - September 07, 2010
Habari ID: 1989355
Kikao cha 'Uislamu, Ulaya na Utandawazi' kimepangwa kufanyika tarehe 8 na 9 za mwezi huu wa Septemba huko mjini Paris. Kikao hicho kimeandaliwa na Jumuiya ya Utamaduni wa Kiislamu ya Ufaransa.
Kwa mujibu wa Saphirnews kikao hicho kitahudhuriwa na waandishi wa vitabu na habari, wahadhiri, wanafikra, wanazuoni wa Kiislamu na wasio Waislamu ili kuchunguza nafasi ya taasisi na mashirika ya utamaduni ya Kiislamu katika ulimwengu wa sasa.
Washiriki wa kikao hicho watapewa fursa ya kutoa misimamo na maoni yao kuhusiana na nafasi ya Uislamu barani Ulaya na umuhimu wa utandawazi kwa Waislamu. Lengo la kikao hicho limetajwa kuwa ni kuandaliwa uwanja wa kufanyika mazungumzo huru kuhusu Uislamu na kuarifishwa utamaduni wa Kiislamu kwa kuheshimiwa fikra za upande wa pili.
Vilevile kikao hicho cha siku mbili kitajadili maudhui nyingine kadhaa zikiwemo za ulimwengu wa Kiislamu na Ulaya, mgongano wa tamaduni, mtengano wa Ulaya na ulimwengu wa Kiislamu; sababu na matokeo yake, vizuizi vinavyozuia kuimarika kwa uhusiano wa Waislamu na nchi za Magharibi. 649167
captcha