Kadyrov amewaambia waandishi habari kwamba amekuwa na matarajio ya kujenga msikiti mkubwa kuliko yote dunia huko Chechnya. Amesema yeye ni mtumishi wa Uislamu na Waislamu na kwamba atawathibitishia walimwengu kwamba Uislamu ni dini ya amani.
Rais Ramzan Kadyrov wa Chechnya amesema awali jamhuri hiyo ilijenga msikiti mkubwa zaidi barani Ulaya na sasa imeazimia kujenga eneo kubwa zaidi la ibada dunia katika jamhuri hiyo.
Rais wa Chechnya hakutoa taarifa kamili kuhusu lini ujenzi wa msikiti huo utakapoanza au gharama za ujenzi huo na ramani yake. 650049