IQNA

Kufanyika kongamano la Uislamu na Waislamu nchini Marekani

17:44 - September 08, 2010
Habari ID: 1990195
Kongamano na Uislamu na Waislamu Nchini Marekani linalodhaminiwa na Chuo cha Kiislamu cha Chicaco kwa ushirikiano wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC limepangwa kufanyika nchini humo tarehe 28 hadi 30 za mwezi huu wa Septemba.
Kwa mujibu wa shirika la Dunyabulteni kongamano hilo la siku tatu litafunguliwa kwa hotuba ya Ekmeleddin Ihsanoglu, Katibu Mkuu wa OIC na litachunguza masuala mbalimbali yanayohusiana na maisha ya Waislamu nchini Marekani.
Masuala mengine yatakayojadiliwa ni pamoja na nafasi ya OIC ulimwenguni na athari zake kwa Waislamu wa Marekani, siasa za nje za Marekani na ulimwengu wa Kiislamu, taathira ya Uislamu kwa muundo wa kijamii wa Waislamu wa Marekani na taswira kuhusu mustakbali wa masomo, utamaduni na siasa za Waislamu wa nchi hiyo.
Wawakilishi wa jumuiya mbalimbali za Kiislamu za Marekani zikiwemo za Baraza la Uhusiano wa Uislamu na Marekani CAIR, Muungano wa Waislamu wa Marekani Kaskazini MANA, wanafikra na wanazuoni wa Kiislamu pamoja na wajumbe wa OIC wamealikwa kushiriki katika kongamano hilo. 650076
captcha