Kwa mujibu wa shirika la habari la Raswid, tamasha hilo la Qur'ani litafanyika katika Msikiti wa Imam Hussein (as) katika mji huo ambapo wasomaji mashuhuri wa Qur'ani na makundi ya kasida kutoka katika eneo la wakazi wengi wa Kishia la as-Sharqiyya wanatarajiwa kushiriki.
Usomaji Qur'ani Tukufu, kasida na mashairi ya kimaanawi ni miongoni mwa mambo yatakayotekelezwa katika ratiba ya tamasha hilo.
Ali Hammad, Nassir Bu Abdullah, Othman al-Kini, Muhammad Fauzi al-Faraj na Swabir al-Mudh'ha wasomaji mashuhuri wa Qur'ani na wasomaji mashairi ya kuwasifu Ahlul Beit (as) ni miongoni mwa watu watakaoshiriki katika tamasha hilo la Qur'ani. Tamasha hilo limepangwa kuanza leo saa nne usiku. 650294