Kwa mujibu wa jarida la kila wiki la Capital la Ethiopia, Benki Kuu ya Ethiopia inafanya mazungumzo na benki za nchi hiyo kwa lengo la kutekeleza huduma za kibenki na kibiashara kwa mujibu wa sheria za Kiislamu.
Kwa mujibu wa sheria hiyo, benki za kitaifa na kigeni zilizo nchini Ethiopia zimeidhinishwa kutoa huduma kwa mujibu wa sheria za Kiislamu. Aidha raia wa Ethiopia wana haki ya kuanzisha Benki za Kiislamu.
650480