Ayatullah Khamenei, ameyasema hayo Ijumaa tarehe Mosi Shawwal mwaka 1431 H alipoonana na viongozi wa Jamhuri ya Kiislamu, mabalozi wa nchi za Kiislamu waliopo Tehran na wananchi wa matabaka mbali mbali kwa mnasaba wa sikukuu ya Idi ‘l-Fitr.
Kiongozi Muadhamu amesema kwenye mkutano huo kwamba somo kubwa kabisa linalopatikana kwenye Idil ‘l-Fitr ni mshikamano na umoja katika ulimwengu wa Kiislamu. Amesisitiza kuwa mataifa ya Kiislamu yanapaswa kuzidi kukurubiana siku baada ya siku na yajitahidi kupigania umoja na mshikamano baina yao kadiri yanavyoweza kwani njia pekee ya kukabiliana na kambi ya maadui wa Uislamu ni kuunda kambi iliyoshikana ya umma wa Kiislamu.
Amesema, safu madhubuti na zilizoshikamana za Waislamu katika sala za Idi ‘l-Fitr ni moja ya madhihirisho ya unyenyekevu wa Waislamu mbele ya Mola Muumba na zinaonyesha mfungamano wa kimaanawi na kimoyo wa Waislamu.
Ameongeza kuwa, safu hiyo moja na iliyoshikamana ya umma wa Kiislamu inabidi ishuhudiwe katika masuala yote yanayouhusu ulimwengu wa Kiislamu ili kwa kuimarisha na kuunganisha nguvu na fikra zao, Waislamu waweze kukabiliana vilivyo na kambi kubwa ya maadui wa Uislamu.
Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ijumaa, Septemba 10, 2010, ameonana na viongozi wa Jamhuri ya Kiislamu, mabalozi wa nchi za Kiislamu waliopo Tehran na wananchi wa matabaka mbali mbali kwa mnasaba wa sikukuu ya Idi ‘l-Fitr.
Kiongozi Muadhamu amesema kwenye mkutano huo kwamba somo kubwa kabisa linalopatikana kwenye Idil ‘l-Fitr ni mshikamano na umoja katika ulimwengu wa Kiislamu. Amesisitiza kuwa mataifa ya Kiislamu yanapaswa kuzidi kukurubiana siku baada ya siku na yajitahidi kupigania umoja na mshikamano baina yao kadiri yanavyoweza kwani njia pekee ya kukabiliana na kambi ya maadui wa Uislamu ni kuunda kambi iliyoshikana ya umma wa Kiislamu.
Amesema, safu madhubuti na zilizoshikamana za Waislamu katika sala za Idi ‘l-Fitr ni moja ya madhihirisho ya unyenyekevu wa Waislamu mbele ya Mola Muumba na zinaonyesha mfungamano wa kimaanawi na kimoyo wa Waislamu.
Ameongeza kuwa, safu hiyo moja na iliyoshikamana ya umma wa Kiislamu inabidi ishuhudiwe katika masuala yote yanayouhusu ulimwengu wa Kiislamu ili kwa kuimarisha na kuunganisha nguvu na fikra zao, Waislamu waweze kukabiliana vilivyo na kambi kubwa ya maadui wa Uislamu.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amekumbusha kuwa kambi ya maadui ina uadui na Waislamu wote bila ya kujali tofauti zao za kimadhehebu na kuongeza kuwa, taswira waliyo nayo wale watu wanaodhani kuwa maadui wana urafiki na baadhi ya Waislamu na wana uadui na baadhi nyingine ya Waislamu ni taswira ghalati kwani ukweli wa mambo ni kuwa maadui wa Uislamu hawataki kusikia hata jina tu la Uislamu na wana uadui wa dhati na asili yenyewe ya Uislamu ambao unasimama kidete kukabiliana na ubeberu wao.
Ayatullah Udhma Khamenei ameashiria pia juu ya mwamko unaozidi kuongezeka wa umma wa Kiislamu na kuongeza kuwa, mwamko na mtazamo mpana walio nao Waislamu kuhusu kadhia ya Palestina ni mfano wa wazi unaoonyesha kuwa Waislamu wanazidi kuamka siku baada ya siku.
Amesema, leo hii taifa kubwa la Iran ni kigezo cha mataifa mengine ya Kiislamu na linafuatilia kwa mwamko kamili matukio ya duniani na masuala yote ya ulimwengu wa Kiislamu.
Ameongeza kuwa, kujitokeza kwa wingi wananchi wa Iran katika maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds ni uthibitisho kuwa taifa la Iran linayapa umuhimu mkubwa masuala ya ulimwengu wa Kiislamu.
Amesisitiza kuwa, hii ndiyo ile njia ambayo Imam Khomeini (quddisa sirruh) aliianzisha kwa ajili ya walimwengu na kwamba vitisho, uadui na chuki za maadui haziwezi kulikwamisha taifa la Iran katika njia yake hiyo.
Mwanzoni mwa mkutano huo, Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametoa mkono wa baraka na fanaka kwa mnasaba wa sikukuu ya Idi ‘l-Fitr na kusema kuwa miongoni mwa matunda na baraka za mwezi wa Ramadhani ni taqwa.
Amesisitiza kuwa, taifa la Iran litaendelea kutumia silaha yake ya taqwa kupigania uadilifu, usafi wa moyo na kusimama kidete mbele ya maadui.
Rais Ahmadinejad vile vile amegusia uamuzi wa mtu mmoja jahili na mpumbavu aliyedai kuwa atachoma moto nakala za Kitabu Kitakatifu cha Qur'ani Tukufu katika maadhimisho ya Septemba 11 huko nchini Marekani na kuongeza kuwa, Wazayuni na waungaji mkono wao hivi sasa wamo katika mkondo wa kuporomoka na kutoweka kabisa na kwamba vitendo kama vya kasisi huyo jahili wa Kimarekani si tu haviwezi kuwaokoa, lakini pia vitaongeza maradufu kasi yao ya kuangamia.
652155