Viongozi wa Kanisa la Westboro Paptist katika mji wa Topeka jimboni Kansas wamesisitiza kuwa watachoma moto Qur'ani Tukufu. Hii ni katika hali ambayo suala la kuchoma moto kitabu hicho kitukufu sasa limekuwa mtindo kwa makanisa ya Marekani na hujuma na mashambulio dhidi ya matukufu ya Kiislamu yamepamba moto.
Kanisa hilo linalojifaharisha kwa kupinga mafundisho ya dini za Kiislamu, Kikristo na Kiyahudi liko nje ya sheria za makanisa ya Marekani na muasisi wake ana chuki kubwa dhidi ya mafundisho ya dini.
Katika upande mwingine vyombo mbalimbali vya habari vimeripoti kuwa baadhi ya raia wa Marekani jana walichoma moto nakala za kitabu kitakatifu cha Qur'ani katika miji mbalimbali ya nchi hiyo na kurusha hewani filamu za kitendo hicho kiovu.
Mapema leo Mmarekani mmoja alitoka hadharani na kurarua kisha kukichoma moto kitabu cha Qur'ani mbele ya kamera za waandishi habari na wananchi waliokuwa katika eneo kunakojengwa majumba mapacha mjini New York.
Makumi ya watu walichukua picha za kitendo hicho kiovu kwa kamera na simu zao za mkononi na kuzituma kwa kanali za televisheni za Marekani na mitandao ya intaneti.
La kushangaza ni kuwa Polisi ya Federali ya Marekani FBI awali ilimuachia mhalifu huyo akitekeleza kwa uhuru kamili kitendo hicho kiovu na kuwaacha watu wakichukua picha za tukio hilo na baada ya kupita muda walimuondoa mhalifu huyo mahala hapo kwa heshima kamili.
Hadi sasa filamu zisizopungua 11 za kuchomwa moto Qur'ani katika miji mbalimbali ya Marekani zimeonyeshwa katika mtandao wa YouTube peke yake. 652639