IQNA

Ahmad Nuaina:

Mustafa Ismail ndiye kigezo changu

15:50 - September 12, 2010
Habari ID: 1992025
Mustafa Ismail ni miongoni mwa shakhsia na makari wa Qur'ani waliokuwa na taathira kubwa katika maisha yangu ya Kiqur'ani na kiraa yake imesaidia sana katika kustawisha usomaji wangu.
Hayo yamesemwa na kari mashuhuri wa Misri Ahmad Ahmad Nuaina katika mahojiano yake na shirika la habari la IQNA na kuongeza kuwa alipoanza kusoma Qur'ani alikuwa akikalidi kiraa ya Sheikh Mustafa Ismail na kutegemea sikio usomaji wake.
Amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Afrika Kusini, Uturuki, Malaysia na Imarati ni miongoni mwa nchi zinazovutiwa mno na kiraa za wasomaji mashuhuri katika ulimwengu wa Kiislamu na mahudhurio makubwa ya watu wa nchi hizo katika majlisi za Qur'ani hayana maana ya kuwapenda makari hao bali ni ishara ya mapenzi yao makubwa kwa kitabu kitukufu cha Qur'ani.
Akijibu swali kwamba ni kwa nini hakuna hata kanali moja ya televisheni ya Qur'ani nchini Misri licha ya kuwapo wasomaji nyota na mashuhuri wa Qur'ani nchini humo? Ahmad Nuaina amesema: "Redio Qur'ani ya Misri imekuwa na nafasi kubwa katika kuwaarifisha makari wa Misri na kwamba anatarajia kuwa mpango wa kuanzisha televisheni ya Qur'ani utatekelezwa.
Msomaji huyo mashuhuri wa Misri amesema anapendelea mno kusikiliza Qur'ani inayosomwa kwa kuzingatia sheria zake na kwamba kisomo kama hicho huwa kana kinasomwa na Malaika.
Ahmad Nuaina ni daktari, kari na refa wa kimataifa wa Qur'ani Tukufu na amesimamia mara kadhaa mashindano ya kimataifa ya Qur'ani nchini Iran. 652749

captcha