IQNA

Mwenyezi Mungu atailinda Qur'ani

11:11 - September 13, 2010
Habari ID: 1992222
Wasomaji wakongwe wa Qur'ani Tukufu nchini Iran wamezungumzia maafa ya kuvunjiwa heshima kitabu kitukufu cha Qur'ani kwa kuchomwa moto nchini Marekani wakisema kuwa Mwenyezi Mungu mwenyewe (SW) ndiye atakayeilinda Qur'ani Tukufu.
Wanasema kwa mujibu wa aya 9 ya suratul Hijr inayosema: "Hakika Sisi ndio tulioteremsha Qur'ani hii na hakika Sisi ndio tutakaoilinda."
Msomaji mkongwe wa Qur'ani wa Iran Abdul Rasul Abai ambaye pia ni refa wa kimataifa wa mashindano ya Qur'ani amelaani kitendo kiovu cha kuchomwa moto Qur'ani nchini Marekani katika kumbukumbu ya mashambulizi ya kigaidi ya tarehe 11 Septemba na akasema: "Qur'ani ni haki na kweli na maadui wa Uislamu wanalivua hilo vyema na wanatambua kwamba Mtume Muhammad (saw) ametuambia mtakapozongwa na fitina kimbilieni Qur'ani."
Ameongeza kuwa maadui wa Uislamu pia wanaelewa thamani na utukufu wa Qur'ani na ni kwa sababu hiyo ndiyo maana wana kinyongo na chuki na kitabu hicho cha Mwenyezi Mungu. Abai amesoma aya ya 54 ya suratul Al Imran inayosema: "Na wamefanya hila, na Mwenyezi Mungu amezipindua hila zao, na Yeye Mwenyezi Mungu ndiye mbora wa kupindua hila za watu waovu."
Abdul Rasul Abai amesema maadui wa Uislamu na Qur'ani wana nia ya kuzima taa na nuru ya Qur'ani bila ya kutambua kwamba nuru ya kitabu hicho cha Mwenyezi Mungu haiwezi kuzimwa kama inavyosema aya ya 39 ya suratul Tauba inayosema: "Wanataka kuzima nuru ya Mwenyezi Mungu kwa vinywa vyao, lakini Mwenyezi Mungu amekataa isipokuwa kutimiza nuru yake ijapokuwa makafiri wanachukia." Ameongeza kuwa maadui wa Uislamu wanataka kuzima nuru ya Mwenyezi Mungu na Qur'ani na kuondoa mafundisho ya kitabu hicho kati ya Waislamu.
Karii huyo mkongwe wa Iran amesema Qur'ani ni kitabu kitakatifu kwa Waislamu kote duniani na hapana shaka kitendo cha kukivunjia heshima kitabu hicho huko Marekani kimewachukiza wafuasi wote wa dini hiyo. 652946
captcha