Baada ya makasisi wawili wa jimbo la Tennessee nchini Marekani kuchoma kitabu kitakatifu cha Waislamu Qur'ani, siku ya Jumamosi Septemba na hivyo kuamsha hasira ya Waislamu katika pembe mbalimbali za dunia, wimbi la kubezwa kitabu hicho na maadui wa Uislamu lingali linaendelea.
Wakili mmoja raia wa Australia amechanachana kurasa za kitabu hicho pamoja na Biblia na kisha kuzichoma moto. Kwa mujibu wa shirika la habari la France Press wakili huyo kwa jina la Alex Stewart ambaye ni mwanachama wa kundi moja la kikafiri alikunja kurasa hizo alizochana mfano wa sigara na kisha kuzichoma moto.
Kafiri huyo alipiga picha kitendo chake hicho cha aibu na kisha kuuliza ni kitabu gani kati ya vitabu viwili hivyo kilikuwa kikiungua vizuri zaidi! Mtu huyo muovu alituma picha hizo za video katika tovuti ya Youtube, ingawa zilifutwa kwenye tovuti hiyo baadaye.
Naibu mkuu wa Chuo cha Ufundi cha Queensland nchini Astralia ambako ndiko anakofanyakazi wakili huyo, amekasirishwa mno na kitendo cha wakili huyo.
Sheikh Muhammad Wahid, Mkuu wa Muungano wa Kiislamu wa Australia amelaani kitendo hicho cha kubeza Qur'ani na kusema kuwa jambo hilo limewaudhi sana Waislamu. Katika kutoa radiamali yake kuhusiana na malalamiko yanayofanywa na Waislamu ulimwenguni kuhusiana na dharau dhidi ya matukufu ya Kiislamu, Stewart amesema katika jarida la makafiri la Brisbane Atheist kuwa ametengeneza mkanda huo wa video kwa lengo la kujifurahisha tu na kwamba hakuna mtu yoyote aliye na haki ya kulalamikia jambo hilo. 653582