IQNA

Juhudi za mtangazaji wa Marekani za kutaka kuchoma moto Qur'ani

11:15 - September 15, 2010
Habari ID: 1993990
Licha ya Terry Jones wa Florida kufutilia mbali uamuzi wake wa kutaka kuchoma Qur'ani mtangazi mmoja wa redio katika jimbo la Georgia alisafiri hivi karibuni hadi katika jimbo la Florida kwa lengo la kuchoma moto Qur'ani.
Kwa mujibu wa tovuti ya Radio info, polisi ya mji wa Gainesville katika jimbo la Florida walipoona watu wamemzunguka mtu mmoja aliyekuwa akijiarifisha kwa jina la Sebastian Bigboy na kwamba ni mhandisi aliyehitimu masomo katika Chuo Kikuu cha Georgia, walitambua kusudio lake la kutaka kuchoma Qur'ani na hivyo kulazimika kumpokonya Qur'ani aliyokuwa amebeba mkononi. Mtu huyo aliyejiarifisha kwa jina bandia lililotajwa hapo juu kwa hakika alikuwa ni mtangazaji mashuhrui wa kituo cha redio cha Rock Atlanta. Licha ya hayo lakini mhalifu huyo aliruhusiwa kuondoka katika eneo hilo bila ya kuchukulia hatua yoyote ya kisheria. Licha ya Terry Jones wa kanisa la Dove World Outreach Center la mjini Florida kufutilia mbali uamuzi wake wa kutaka kuchama Qur'ani lakini raia kadhaa wa Marekani wakiwemo makasisi wawili wa jimbo la Tennessee wamekibeza kitabu hicho kwa kukichana na kisha kukichoma moto kwa manasaba wa tukio la Septemba 11. Matukio kama hayo yametokea katika maneo mengine ya Marekani na pia nchini Australia. 653765
captcha