IQNA

Mbunge wa Kongresi ya Marekani:

Wamarekani wengi hawaujui Uislamu

19:27 - September 14, 2010
Habari ID: 1994080
Mbunge wa kwanza Muislamu katika Kongresi ya Marekani Maurice Keith Ellison amesema kuwa Wamarekani wengi hawajui lolote kuhusu dini ya Kiislamu.
Keith Ellison amesema ameyasema hayo baada ya Wakristo wenye misimamo mikali wa Marekani kuchoma moto kitabu kitakatifu cha Qur’ani katika kumbukumbu ya matukio ya Septemba 11. Maurice Keith Ellison amewataka raia wa Marekani kwenda misikitini, makanisani na katika nyumba za ibada za Mayahudi ili kujua mafundisho ya dini hususan Uislamu.
Mbunge huyo wa Kongresi ya Marekani amesema kuwa dini ya Kiislamu haihusiki na ugaidi na kwamba watu waliohusika na mashambulizi ya Septemba 11 hawana mfungamano wowote na Uislamu.
Mbunge huyo Muislamu amesisitiza juu ya udharura wa kuimarishwa na kulindwa uhuru wa kiraia katika jamii ya Marekani.
Wakati huo huo Baraza la Uhusiano wa Uislamu na Marekani CAIR limetangaza kuwa litaanza kugawa nakala milioni moja za kitabu kitakatifu cha Qur’ani nchini humo kama jibu la kuchomwa moto kitabu hicho cha Mwenyezi Mungu huko Marekani. 654454
captcha